• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

KATAVI KUANZA KUTUMIA UMEME WA GRID YA TAIFA MEI 20,2025.

Posted on: May 15th, 2025

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na ujenzi wa vituo vya kupokea, kupoza na kusambaza umeme Inyonga chenye uwezo wa 15MVA  katika eneo la Utende wilayani Mlele mkoani hapa.

Akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na miradi ya kimikakati leo Mei 14, 2025 wilayani Mlele Mhe. Mrindoko amesema Mradi huo unatarajiwa kuanza kutumika ifikapo Mei 20, 2025 ambapo pamoja na kuondoa changamoto ya kukatika kwa umeme  utaongeza ari ya uwekezaji kutokana na kuwa gharama za uendeshaji wa miundombinu ya uzalishaji inayotegemea umeme itapungua.

Picha: Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na ujenzi wa vituo vya kupokea, kupoza na kusambaza umeme Inyonga chenye uwezo wa 15MVA  katika eneo la Utende wilayani Mlele.

Mkoa wa Katavi  unatekeleza mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msonyo wa kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Katavi na ujenzi wa vituo vya kupokea, kupoza na kusambaza umeme katika vituo vya Ipole chenye uwezo wa 15MVA, Inyonga chenye uwezo wa 15MVA na Mpanda chenye uwezo wa 35MVA.

"Awali wawekezaji walikuwa na kikwazo cha umeme kwa sababu hakukuwa na kituo cha kupozea umeme katika mkoa wetu na sasa changamoto imeisha hivyo kila mwananchi awaze kuwekeza katika maeneo tofauti ili kuweza kujijenga zaidi kiuchumi,".

PICHA: Muonekano wa eneo la mradi wa kupokea, kupoza na kusambaza umeme Inyonga chenye uwezo wa 15MVA na Mpanda chenye uwezo wa 35MVA unaotarajiwa kuanza kutumika Mei 20, mwaka huu.

Ameongeza kuwa ni wajibu wa wananchi kuilinda na kuitunza miundombinu uliyojengwa ili isichakae mapema pamoja na kuwahakikishia wananchi kuwa serikali kupitia wakala wa umeme vijijini Rea imeendelea kufikisha huduma ya umeme katika maeneo na vijiji na sasa hudumia hiyo imefika katika vitongoji hivyo ni wajibu wa wananchi kutumua fursa hiyo kujiimarisha kiuchumi kupitia umeme katika vitongoji vyao.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa niaba ya meneja wa Tanescomkoa wa Katavi Mhandisi Dalali Lunyamila amesema mradi unatekelezwa na serikali kwa fedha za ndani  ambapo gharama yake ni bilioni 164.15 ulioanza Septemba 2022 na unatarajiwa kukamilika Juni 2025 huku utekelezaji ukiwa umefikia 96%.

"Mradi huu mara baada ya kukamilika utawezeshaKuunganisha Mkoa wa Katavi na umeme wa grid ya Taifa.itawezesha wawekezaji wa ndani na nje kuwa na uhakika wa kupata umeme kwa maendeleo ya Viwanda, kilimo na matumizi ya kijamii pia mapato kwa shirika la umeme Tanzania yataongezeka kwa kuunganisha wateja wengi zaidi na hivyo kujikwamua kiuchumi". Amesema Lunyamila.



Mwisho.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC MRINDOKO ATOA WITO KWA VIONGOZI KUHAMASISHA MATUMIZI YA CHAKULA CHENYE VIRUTUBISHI ILI KUTOKOMEZA UDUMAVU.

    June 10, 2025
  • RC MRINDOKO AZINDUA MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA NA MAZAO MENGINE KWA MWAKA 2025/26

    June 09, 2025
  • RC MRINDOKO AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA KATAVI, ATOA WITO WA AMANI NA USHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025.

    June 05, 2025
  • JAJI MKUU WA TANZANIA ASISITIZA UADILIFU NA USHIRIKIANO WA WADAU KATIKA UTOAJI HAKI.

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved