Na:John Mganga –Katavi RS
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko ametoa wito kwa Wafugaji Wadau mbalimbali wazalishaji wa bidhaa za Maziwa pamoja na Wananchi ndani na Nje ya Mkoa wa Katavi kushiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Siku ya Wiki ya Maziwa yanayotarajiwa kuanza rasmi siku ya Tarehe 27 Mwezi Mei 2022 na kumalizika Tarehe 01 Juni 2022.
Mh.Mrindoko amesema Mkoa wa Katavi umepewa heshima kwa mara nyingine tena kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya Siku ya Maziwa Kitaifa na kwamba hatua hiyo ni fursa kwa Wadau wazalishaji wa bidhaa za Maziwa pamoja na Wananchi Mkoani Katavi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwae Mhe.Mrindoko amesema Maadhimisho hayo yatafanyika katika Uwanja wa CCM azimio ndani ya Manispaa ya Mpanda.
Amesema lengo la madhimisho hayo kwa kila mwaka ni kufanya uelimishaji endelevu kwa wadau mbalimbali na Wananchi kuhusu umuhimu wa Unywaji wa Maziwa pamoja na umuhimu wa unywaji wa maziwa yaliyosindikwa pamoja na kuelezea umuhimu wake katika Lishe.
Mhe.Mkuu wa Mkoa amesema lengo la Mkoa wa Katavi ni kuhakikisha kuwa unaongeza Uzalishaji wa Maziwa kwa wingi pamoja na kupanua wigo wa uanzishwaji wa Viwanda vya Usindikaji wa maziwa.
Katika maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zinatarajiwa kufanyika ikiwa ni pamoja na maonyesho ya bidhaa mbalimbali za Maziwa,Elimu kuhsu namna bora ya kusindika Maziwa.
Aidha maadhimisho hayo yataambatana na shughuli ya kutembelea mashamba ya wafugaji kwa lengo la kuwaelimisha matumizi mbalimbali ya teknolojia ya kisasa ya Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa pamoja na upatikanaji wake.
Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa Kitaifa Mkoani Katavi yanabeba Kaulimbiu inayosema Kunywa Maziwa yaliyosindikwa Tanzania Kwa Lishe Bora na Salama.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved