MAMLAKA YA MAWALIANO KWA WOTE YAKABIDHI MSADA WA COMPUTER ZA MILIONI 46 KWA MANISPAA YA MPANDA.
Mamlaka ya Mawasiliano kwa wote imekabidhi msaada wa COMPUTER 25 zenye thamani ya shilingi milioni 46 zitakazotumika kwa ajiri ya Shule za Sekondari za Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda zilizokuwa na ukosefu wa computer.
Msaada huo umekabidhiwa leo na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mwandisi Atashasta Nditiye kwa Manispaa ya Mpanda wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda ambapo msaada huo alikabidhiwa Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi kwa niaba ya Manispaa ya Mpanda .
Akizungumza kwenye hafla hiyo Naibu Waziri Nditiye alieleza kuwa Serikali imetoa msaada huo wa Computer ili wanafunzi wanao soma kwenye shule za Sekondari waweze kuzitumia kwa ajiri ya matumizi ya kujifunzia na kwa ajiri ya matumizi ya shule .
Alifafanua kuwa Shule za Sekondari za Manispaa hiyo zilikuwa na ukosefu wa Computer za matumizi ya shule hali ambayo imekuwa ikisababisha shule kutumia computer za Walimu binafsi kwa ajiri ya matumizi ya shule au kwenda kufanyia kazi kwenye steshenali .
Alieleza kuwa ni jambo la hatari sana shughuli za shule kwenda kufanyia kwenye steshenali na kwenye Computer za Walimu binafsi kwani sio watu wote ambao wanaweza kuwa wanatunza siri.
Alisema msadaa huo umetolewa na Mamlaka ya Mawasiliano kwa wote ambayo ipo chini ya Wizara yake kufuatia maombi yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastiani Kapufi na wataendelea kutoa misaada kama hiyo kwenye shule mbalimbali hapa nchini kwani mahitaji hayo bado yanahitajika na hata kwa Manispaa ya Mpanda bado hazitoshi .
Aidha alieleza kuwa Serikali itaendelea kuwashawishi wawekezaji waendelee kuweka
minara ya mawasiliano ili mawasiliano yasikosekane kwenye maeneo yote ambayo hayana mawasiliano hapa nchini.
Aliwakata Watanzania kutumia vizuri mawasiliano kwani wapo baadhi ya watu wamekuwa wakitumia vibaya mawasiliano na wanaotumia vibaya mawasiliano Serikali itaendelea kuwachukulia hatua.
Hivyo aliwaonya wanao tumia vibaya mitandao waache mara moja kwani kila kinachofanyika kwa nia mbaya kwenye mitandao Serikali inakifahamu na itawakamata wale wote wanaofanya kutapeli watu na kuweka picha za matusi.
Pia ameagiza bodi ya TTCL kwa kuipa mwezi mmoja iwe imefika Mkoani Katavi na kutembelea Ofisi ya Kampuni hiyo ambayo bado inahesabika kuwa ni ofisi ya Wilaya lengo la kuigiza bodi hiyo ni kutaka kuipandisha hadhi ofisi hiyo iwe ya Mkoa kwani ni kitu ambacho hakitawezekana ofisi hiyo kuendelea kuwa ya Wilaya ya Mpanda wakati saa ni Mkoa wa Katavi .
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Abdalla Malela alieleza kuwa Mkoa unahudumia jumla ya vituo viwili vya mkongo wa Taifa ambavyo ni Mpa T/ HOUSE na kituo cha Mishamo vyenye urefu wa kilometa 240 ambapo Kizi Mpanda km 122 na Mpanda Mishamo Km 118.
Alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili shirika la TTCL katika kuhudumia mkongo wa Taifa kuwa ni hujuma zinazosababishwa na baadhi ya wananchi wasiowaaminifu ambao wamekuwa wakisababisha mawasiliano kukatika katika Mkoa wa Katavi na Nchi za jirani .
Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Mpanda Enelia Lutungulu alisema Manispaa hiyo ina jumla ya Shule 14 za Sekondari zikiwemo 10 za Serikali na nne zisizo za Serikali, Shule za Sekondari na msingi kwenye Manispaa hiyo zina mahitaji makubwa sana ya Computer kutokana na maendeleo ya Sayansi na Tekinolojia na Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano kwa kutumia computer.
Hivyo kuleta ugumu wa utendaji kazi wa kila siku ukizingatia kuwa upokeaji na utoaji wa taarifa ni wa kila mara hivyo msaada huo utasaidia kupunguza tatizo hilo kwenye shule za Sekondari.
Akipokea msaada huo Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Sebastian Kapufi alishukuru na kusema asante na wala hata choka kuomba tena msaada kama huo kwani kutokana na mahitaji yalipo anatumia nafasi hiyo kuomba tena msaada kama huo .
Alieleza kuwa shule binafsi nazo ni wadau wakubwa kwenye maendeleo ya elimu hivyo wakati wa ugawaji wa computer hizo hauta zibagua shule hizo nazo pia watanufaika na msaada huo .
Mkurugenzi wa mfuko wa mawasiliano kwa wote Albarti Richald alieleza kuwa kwa mwaka huu wamepanga kutoa msaada kwenye shule 150.
Mbali ya kutoa misaada ya aina hiyo pia wamekuwa wakitowa mafunzo ya Tehama kwa baadhi ya walimu ambapo wakisha patiwa mafunzo huenda kuwafundisha walimu wenzao kwenye shule zao.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved