• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

Serikali kuhakiki upya ugawaji maeneo yenye Migogoro Katavi,RC aiomba tume kuharakisha utatuzi.

Posted on: October 12th, 2022

Mwenyekiti wa Tume ya Mawaziri Nane iliyoundwa kutatua migogoro ya Ardhi Mhe.Mashimba Ndaki akizungumza katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda Mara baada ya kuwasili Mkoani Katavi kwa ajili ya ziara kutatua migogoro ya ardhi.

Serikali imeridhia kufanya upya uhakiki wa ugawaji wa maeneo ambayo yameonekana kuwa na migogoro ya ardhi mkoani Katavi.

Akizungumza baada ya kutembelea baadhi ya maeneo hayo ikiwemo eneo la Visima Viwili lililopo katika Kata ya Kasekese wilayani Tanganyika,Mwenyeketi wa kamati ya mawaziri nane wa kisekta ambaye ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ameelekeza kufanyika upya tathmini kwa maeneo yote Mkoani Katavi yenye migogoro ya mipaka baina ya Wananchi na Mamlaka za Uhifadhi ili kuja na suluhu ya kudumu ya kuondoa Migogoro hiyo

Aidha Mhe.Ndaki amewaomba Wananchi Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi  kuepuka kuendelea kufanya shughuli za  makazi katika maeneo ambayo hawana uhakika wa kuendelea kuishi kusudi kuepuka usumbufu na wakati mwingine hasara zisizokuwa na ulazima.

Awali akizungumza wakati wa utambulisho Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko aliiomba tume hiyo   ya Mawaziri Nane inayozunguka Nchi nzima   kutatua Migogoro mbalimbali ya ardhi kuharakisha utatuzi wa migogoro mbalimbali ya ardhi inayoendelea baina ya Wananchi na maeneo ya hifadhi Mkoani Katavi ili kutoa fursa kwa Wananchi kufanya maandalizi ya mashamba kwa wakati ili kuendana na msimu wa Mvua ambao umekaribia.

Kwa upande wao wananchi wameomba kamati hiyo kushughulikia kwa haraka jambo hilo ambalo limekuwa likisababisha migogoro inayojirudiarudia.

Kamati hiyo ya Wizara nane za kisekta imeundwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Kilimo na Ushirika, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira)kwa ajili ya kutembelea maeneo yenye migogoro ya ardhi nchini na baadae kutoa mapendekezo ya namna ya kusuluhisha migogoro hiyo.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Katavi aongoza Wananchi kupanda Miti,ahimiza utunzaji wa mazingira,vyanzo vya Maji,akemea vikali shughulli za kibinadamu katika vyanzo vya Maji.

    January 26, 2023
  • RC Kataci aongoza Wananchi kupanda Miti,Ahimiza utunzaji wa mazingira,vyanzo vya Maji,akemea vikali shughulli za kibinadamu katika vyanzo vya Maji.

    January 26, 2023
  • RC Katavi akabidhi pikipiki 8 kwa Maafisa Tarafa. Awataka kutumia vyombo hivyo kufuatilia Ugawaji wa Mbolea,Uripoti wa Wanafunzi Mashuleni.

    January 13, 2023
  • KATAVI WATEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU, KITUO CHA AFYA MAJIMOTO CHAANZA KUTOA HUDUMA,

    December 30, 2022
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • MWENGE BLOG-KATAVI
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved