• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

Viongozi /Wadau watakiwa kuelekeza nguvu hamasa kwa Wananchi kupima VVU kutambua Afya zao.

Posted on: December 1st, 2022

Pichani:Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw.Hassa Abas Rugwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ys UKIMWI Duniani alipotoa hotuba yake katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kasekese wakati wa maadhimisho ya Siku ya UKIMW Duniani 1 Desemba 2022.


Tanganyika,

Viongozi,Wataalamu pamoja na wadau mbalimbali Mkoani  Katavi wametakiwa kuelekeza nguvu zaidi katika kutoa Elimu juu ya umuhimu wa kupima Virusi vya UKIMWI na kutambua  hali  ya Afya zao ili kuchukua hatua stahiki na kwa wakati ili kuepuka Afya kutetereka.

Rai hiyo imetolewa na Katibu tawala mkoa wa Katavi Bw.Hassan Abas Rugwa katika  maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani iliyoadhimishwa kimkoa  katika Shule  ya msingi Kasekese Kata ya Kasekese Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.

Katibu Tawala Rugwa ameeleza kuwa kutokana na hali ya maambukizi ya VVU kuwa   Asilimia 5.9 katika Mkoa wa Katavi, ambayo ni kiwango cha juu ikilinganishwa na kiwango cha maambukizi ya VVU cha   Taifa ambacho ni Asilimia 4.7 ni muhimu kama Mkoa kujipanga.

“Sisi kama Mkoa tuna kila sababu ya kuhakikisha kuwa tunafanya jitiada za makusudi kushusha kiwango cha maambukizi walau kifikie kiwango chini ya wastani ule wa Taifa kama ambavyo baadhi ya Mikoa ya wenzetu wamefanikiwa kushusha”Alisema Katibu Tawala Rugwa.

Awali akiwasilisha Taarifa mbele ya Mgeni Rasmi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dokta Omari Sukari amesema Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali  umefanikiwa kutekeleza Afua mbalimbali  za kupambana na UKIMWI ambapo Mkoa umefanikiwa kufikia  Malengo ya Tisini na tano ya kwanza kwa Asilimia 111.1,kufikia malengo ya Tisini na tano ya Pili kwa Asilimia 96.9.

Aidha Dokta Sukari ameeleza kuwa Idadi ya Vituo vya kutolea huduma za tiba na malezi kwa watu wanaoishi na VVU (CTC) imeongezeka kutoka vituo 34 mwaka 2020 hadi vituo 51 kufikia Septemba, 2022.

Ameongeza kuwa Idadi ya Vituo vya kutolea huduma za ushauri nasihi na upimaji wa VVU imeongezeka kutoka vituo 76 mwaka 2020 hadi vituo 83 kufikia Septemba 2022.

Katika maadhimisho hayo ya siku ya UKIMWI Duniani iliyobeba kaulimbiu inayosema Imarisha Usawa yamefana katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kasekese ambapo shughuli mbalimbali zikiwemo upimaji wa Afya pamoja na Elimu kuhusu masuala mbalimbali  ya Afya zimefanyika kwa Mafanikio makubwa.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Katavi aongoza Wananchi kupanda Miti,ahimiza utunzaji wa mazingira,vyanzo vya Maji,akemea vikali shughulli za kibinadamu katika vyanzo vya Maji.

    January 26, 2023
  • RC Kataci aongoza Wananchi kupanda Miti,Ahimiza utunzaji wa mazingira,vyanzo vya Maji,akemea vikali shughulli za kibinadamu katika vyanzo vya Maji.

    January 26, 2023
  • RC Katavi akabidhi pikipiki 8 kwa Maafisa Tarafa. Awataka kutumia vyombo hivyo kufuatilia Ugawaji wa Mbolea,Uripoti wa Wanafunzi Mashuleni.

    January 13, 2023
  • KATAVI WATEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU, KITUO CHA AFYA MAJIMOTO CHAANZA KUTOA HUDUMA,

    December 30, 2022
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • MWENGE BLOG-KATAVI
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved