• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

Wakandarasi wa Barabara Katavi watakiwa kuzingatia Weledi,Masharti ya Mikataba.

Posted on: November 11th, 2022

11 Novemba 2022,

Wakandarasi wa Barabara Mkoani Katavi wametakiwa kufanya kazi kwa weledi pamoja na kuzingatia masharti yaliyopo katika mikataba baina yao na Serikali ili thamani ya fedha iweze kuonekana.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Hoza Mrindoko katika hafla ya utiaji  saini mikataba ya ujenzi baina ya Wakala wa Barabara za Miji na Vijijini Nchini TARURA pamoja na Wakandarasi watakaotekeleza kazi za ujenzi,ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya Barabara mkoani humo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 iliyofanyika  katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda.

Jumla ya mikabata 6 imesainiwa yenye thamani ya  zaidi ya shilingi Bilioni 1.5 kati ya TARURA na wakandarasi wa ujenzi wa barabara mkoani Katavi ikiwa ni asilimia 40 ya Bajeti ya Mwaka wa fedha 2022/2023.

"Tarura kwa Mwaka huu wa fedha 2022/2023 imetengewa Bajeti ya shilingi 14,293,366,636 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 30 kati ya miradi hiyo miradi 19 utiaji wake saini ulishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Sulhu Hassan  14 Agosti 2022 jijini Dodoma ammbayo ilikuwa na thamani ya Shilingi 6,646,859,525 ambapo leo hii tumeshuhudia utiaji saini mikataba 6 yenye thamani ya shilingi 1,522,411,920 kati ya TARURA na Wakandarasi wa Ujenzi wa Barabara"Alisema Mkuu wa Mkoa Bi.Mrindoko.

Mkuu wa Mkoa Bi. Mrindoko amewataka TARURA mkoani  Katavi  kushirikiana na TANESCO ,RUWASA na MUWASA  kuhakiki miundombinu iliyopo kwenye hifadhi za barabara na kuiondoa  kwa wakati ili kuepusha ucheleweshaji wa miradi na usumbufu kwa wananchi kukosa huduma.

Aidha Bi Mrindoko amewasisitiza Wakandarasi hao kutoa kipaumbele cha ajira za muda zinazotokana na miradi kwa Wananchi wa maeneo husika paamoja na kuwalipa malipo yao kwa wakati ili Wananchi wa maeneo husika waweze kunufaika na fursa za Miradi hiyo katika maeneo yao.

Awali akitoa taarifa ya mikataba inayosainiwa, meneja wa TARURA  mkoa wa Katavi mhandisi Innocent Mlay amesema wanategemea kujenga barabara mpya za lami zenye urefu wa km 3.73,kufungua barabara mpya km198,ujenzi wa Makalvati 182 na ujenzi wa barabara za changarawe zenye urefu wa km 155.16.

Naye  Mwenyekiti wa umoja wa wakandarasi mkoa wa Katavi Juma Hassan Lumbwe amewataka wakandarasi waliotia saini mikataba hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia viwango na kuisoma mikataba hiyo vizuri ili kuepusha migongano wakati wa utekelezaji wa miradi ya Serikali.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Katavi aongoza Wananchi kupanda Miti,ahimiza utunzaji wa mazingira,vyanzo vya Maji,akemea vikali shughulli za kibinadamu katika vyanzo vya Maji.

    January 26, 2023
  • RC Kataci aongoza Wananchi kupanda Miti,Ahimiza utunzaji wa mazingira,vyanzo vya Maji,akemea vikali shughulli za kibinadamu katika vyanzo vya Maji.

    January 26, 2023
  • RC Katavi akabidhi pikipiki 8 kwa Maafisa Tarafa. Awataka kutumia vyombo hivyo kufuatilia Ugawaji wa Mbolea,Uripoti wa Wanafunzi Mashuleni.

    January 13, 2023
  • KATAVI WATEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU, KITUO CHA AFYA MAJIMOTO CHAANZA KUTOA HUDUMA,

    December 30, 2022
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • MWENGE BLOG-KATAVI
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved