Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Mrindoko amewaelekeza viongozi Mkoani humo kuratibu maadhimisho ya Wiki ya Mwanakatavi ya Kilimo na Utalii kila Mwaka ili kutoa fursa kwa Wananchi kujifunza Teknolojia mbalimbali za kisasa pamoja na fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya Kilimo na Utalii,pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya Kilimo na Utalii kutanua wigo wa masoko ya bidhaa zao.
Bi.Mrindoko ameyaasema hayo 2 Novemba 2022 katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Mwanakatavi ya Kilimo na Utalii yaliyopambwa na maonyesho ya bidhaa mbalimbali za Kilimo pamoja na Utalii yaliyodumu kwa muda wa siku 5 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashato Manispaa ya Mpanda.
Amesema hatua ya kufanya maadhimisho ya Wiki ya Mwanakatavi ya Kilimo na Utalii kila mwaka itasaidia kwa sehemu kubwa Mkoa wa Katavi kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali pamoja na kuleta hamasa ya matumizi ya Teknolojia ya kisasa katika Kilimo na Ufugaji
Aidha Mkuu wa Mkoa Mrindoko amewaelekeza pia Viongozi Mkoani humu wakiwemo Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi kukamilisha Ujenzi wa Uwanja wa Nanenane ulioanza kujengwa katika eneo la Kabungu Wilaya ya Tanganyika ili kutoa fursa kwa Maonyesho ya Mwanakatavi ya Kilimo na Utalii kufanyika katika eneo hilo
Katika hatua nyingine Bi.Mrindoko amewashukuru viongozi na wadau mbalimbali Mkoani humo kwa waliofanikisha kuratibu maadhimisho ya wiki ya Mwanakatavi ya Kilimo na Utalii ambapo pia amewapongeza Wananchi kwa muitikio mkubwa waliouonyesha kushiriki katika Maadhimisho hayo.
Maadhiisho ya Wiki ya Mwanakatavi ya Kilimo na Utalii yamehitimishwa leo baada ya kudumu kwa siku tano tangu kuzinduliwa kwake 28 Oktoba 2022 ambapo shughuli mbalimbali zilifanyika ikiwemo kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii ndani ya Mkoa,uzinduzi wa Filamu ya the Royal Tour,Shindano la kumsaka Mlimbwende wa Utalii Katavi,pamoja na uzinduzi wa Msimu wa Kilimo 2022.
Zaidi ya washiriki 48 zikiwemo Taasisi mbalimbali za Serikali na Mashirika yasiyo ya Kiserikali,Makampuni mbalimbali ya utoaji huduma pamoja na Wajasiriamali wadogo wameshiriki kikamilifu katika maonyesho hayo.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved