• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

Wiki ya Mwanakatavi yazinduliwa rasmi, Wananchi watakiwa kujifunza Fursa Sekta ya Kilimo na Utalii.

Posted on: October 28th, 2022

Pichani:Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe.Filberto Sanga alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko katika uzinduzi wa Wiki ya Mwakakatavi katika uwanja wa Shule ya Msingi Kashato 28 Oktoba 2022

Mpanda.

Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa  kutumia fursa ya maonyesho ya Wiki ya Mwanakatavi kujifunza masuala mbalimbali ya Kilimo na Utalii ili kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo katika Skta ya kilimo na utalii kujikwamua Kiuchumi.

Rai hiyo imtolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bw.Filberto Sanga kwa niaba ya Mkuu wa wa Katavi Bi.Mwanamvua Hoza Mrindoko katika uzinduzi wa  maonyesho ya Kilimo na Utalii ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Mwanakati ya Kilimo na Utalii iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashato Manispaa ya Mpanda

Bw.Sanga amewahimiza Wananchi kutumia vyema manyesho hayo kujifunza fursa mbalimbali katika Sekta ya Kilimo na Utalii zinazopatikana ndani ya Mkoa wa Katavi jambo litakalosaidia kuimarisha uchumi wa Mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Aidha Bw.Sanga ametoa rai kwa Taasisi za Uhifadhi wa Maliasili Mkoani Katavi kuelekeza nguvu ya ziada katika ulinzi wa Maliasili hizo ikiwemo Misitu na Wanyamapori ili kunusuru rasilimali hizo dhidi ya Wavamizi.

Amewataka Maafisa Ugani Mkoani Katavi kuhakikisha wanawasajili wakulima wote kwa kuwa lengo la zoezi hilo licha ya kufanikisha zoezi la uuzaji wa mbolea ya ruzuku pia linalenga kutambua idadi ya Wakulima wote Nchini.

Katika hatua nyingine Bw.Sanga amelitaka shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo Nchini SIDO kujenga uwezo  kwa Wajasiriamali juu ya namna ya kukuza mitaji yao ili kujikwamua na Umasikini.

Awali Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw.Nehemia James katika ufunguzi wa Maonyesho ya Wiki ya Mwanakatavi ya Kilimo na Utalii amesema lengo la maonyesho hayo ni kutoa fursa kwa      Wananchi Mkoani humo kujifunza masuala mbalimbali kuhusu Kilimo na Utalii pamoja na kubaini fursa zilizopo katika Sekta hizo.

Amesema maonyesho  hayo yatadumu kwa muda wa siku 5 baada ya uzinduzi ambapo Washiriki 28 zikiwemo Taasisi mbalimbali za Kiserikali,Mashirika binafsi pamoja na Wajasiriamali wadogo Wanashiriki katika maonyesho hayo.

Aidha katika kuadhimisha Wiki ya Mwanakatavi ya Kilimo na Utalii baada ya uzinduzi Wananchi watapata fursa ya Kushuhudia Shindano la Kusaka Miss Utalii Katavi jioni katika ukumbi wa Mpanda Social ambapo siku ya 30 Oktoba 2022 kutakuwa na tukio la kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii ndani ya Mkoa wa Katavi ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Katavi pamoja na Shamba la Mbuni,ikitafuatiwa na tukio la  Uzinduzi wa Filamu ya The Royal Tour Mkoani Katavi  jioni katika ukumbi wa Mpanda Social.

Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Mlele akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi ametembelea na kukagua mabanda ya maonyesho ya Taasisi mbalimbali na mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na Wajasiriamali wadogo ambapo maadhimisho hayo yanatarajiwa kufungwa rasmi siku ya Tarehe 2 Oktoba 2022.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATAVI KUANZA KUTUMIA UMEME WA GRID YA TAIFA MEI 20,2025.

    May 15, 2025
  • KATAVI YAZIDI KUNG'ARA UUZAJI WA KABONI

    May 13, 2025
  • MABADILIKO YA MAJIMBO YA UCHAGUZI

    May 12, 2025
  • RC MRINDOKO AZINDUA MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU (GAWE) 2025

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved